Beki wa kati wa Simba Salim Mbonde amesema baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti, alipewa mapumziko ya miezi sita mpaka saba yanaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu.
Amesema anatarajia kuanza mazoezi mwanzoni mwa mwezi wa tatu na huenda akarejea dimbani mapema zaidi
Aidha, Mbonde ameushukuru uongozi wa Simba kwa kuendelea kumhudumia kama wachezaji wengine licha ya kutoonekana dimbani kwa muda mrefu kutokana na majeraha hayo
Beki huyo aliyetua Simba akitokea Mtibwa Sugar amekuwa na wakati mgumu tangu aliposajiliwa kutokana na kukabiliwa na majeraha ya mara kwa mara
ADVERTISE HERE