Aussems apania kulipa kisasi kwa Al Ahly Februari 12

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Feb 2019
Aussems apania kulipa kisasi kwa Al Ahly Februari 12

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake bado ina nafasi ya kufanya vizuri na hata kukata tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa kama itashinda michezo miwili ya nyumbani.

Kuhakikisha hilo linafanikiwa Aussems amesema mchezo wa wiki ijayo dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Jumanne ya Februari 12 uwanja wa Taifa ni muhimu kushinda

Licha ya kukiri kuwa Al Ahly ilikuwa bora katika mchezo wa juzi ambao Simba ilikubali kufungwa mabao 5-0, Aussems amesema makosa ya wachezaji wake yalichangia kwa kiasi kikubwa kufungwa idadi hiyo ya mabao

Aussems amesema wakati wa mapumziko walifanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika kipindi cha kwanza na ndio maana kwenye kipindi cha pili hawakuruhusu bao

Amesema wiki ijayo wataendelea walipoishia na kwa kuwa watakuwa wakicheza katika uwanja wa nyumbani, uwezekano wa kushinda mchezo huo upo

Simba inatarajiwa kurejea leo jijini Dar es salaam kuanza maandalizi ya mchezo huo wa raundi ya nne kundi D

Kabla ya kuchuana na Al Ahly, Simba inatarajiwa kucheza na Mwadui Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara utakaopigwa Februari 07 kwenye uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’