Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinarejea nchini leo kutoka Misri kukamilisha ratiba ya mzunguuko wa tatu wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema kutokana na changamoto ya usafiri iliyowakabili wamelazimika kuondoka kwa awamu mbili
Kundi la kwanza liliondoka jana na kundi la pili linalojumuisha wachezaji litaondoka leo Jumatatu
Rweyemamu amewaomba radhi Wana Simba kwa matokeo mabaya waliyoyapata nchini Misri lakini amewataka waendelee kuiunga mkono timu hiyo kwani imedhamiria kufanya vizuri katika michezo inayokuja
ADVERTISE HERE