Maproo wameiangusha Simba michezo miwili iliyopita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Feb 2019
Maproo wameiangusha Simba michezo miwili iliyopita

Kikosi cha Simba kilichoanza jana kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly kilikuwa na wachezaji nane wa kigeni huku watatu pekee wakiwa wazawa

Katika kikosi hicho ni Aishi Manula, Jonas Mkude na Rashid Juma waliokuwa katika kikosi kilichoanza ambao walikuwa wazawa.

Hata hivyo 'maproo' hao wameshindwa kudhihirisha umuhimu wao

Aidha hata katika mchezo dhidi ya Vita Club licha ya idadi kubwa ya maproo, bado Simba haikunufaika na uwepo wao

Moja ya vigezo vilivyotumiwa na TFF katika kuongeza idadi ya usajili wa wachezaji maproo kutoka saba mpaka kumi, ni kuimarisha timu za Tanzania hasa zinazoshiriki michuano mikubwa ya Afrika

Wadau mbalimbali wameushauri uongozi wa klabu ya Simba kuandaa utaratibu mzuri wa kutafuta wachezaji wa kigeni kuliko utaratibu huu wa sasa ambao wachezaji wanaletwa na watu badala ya timu

Simba inapaswa kuwa na kitengo maalum cha kufuatilia mienendo ya wachezaji (scouting) wanaotaka kuwasajili. Timu nyingine huwafuatilia wachezaji mpaka miaka mitatu kabla ya kuwasajili

Hivi karibuni Simba imeleta wachezaji wa kigeni kwa ajili ya kuwafanyia majaribio. Utaratibu huu ulipondwa na wadau kwa kuwa mchezaji mzuri anapaswa awe ameonekana kabla ya kumsajili

Wachezaji hawa wa majaribio wanaweza kufanya vizuri wakati huo lakini wakishasajiliwa, viwango vyao halisi ndio hubakia

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' ana ndoto ya kuifanya Simba kuwa klabu bingwa Afrika. Viongozi wa Simba wanapaswa kutengeneza mfumo mzuri wa kupata wachezaji watakaoweza kufanikisha hili

Mo amekuwa tayari kutumia fedha kuhakikisha Simba inafikia malengo hayo.

Kikosi hiki cha sasa cha Simba kimegharimu takribani Bil 1.3 lakini nadhani bado kinahitaji maboresho makubwa ili kuweza kufikia kiwango cha kuchuana na vigogo wa Afrika katika kuwania ubingwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’