Ligi kuu ya Vodacom imeendelea kwa michezo mitano kupigwa leo.
Yanga imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Prisons huku Singida United ikiilaza Mbeya City mabao 2-1.
Kagera Sugar na Stand United zimetoka suluhu ya bila kufungana wakati Ruvu Shooting imepata ushindi wake wa pili kwa kuilaza Majimaji mabao 2-1.
Mbao FC imeichapa Mwadui FC bao 1-0.
Michezo ya leo haijabadili msimamo wa ligi kwani Yanga imefikisha alama 21 pekee baada kukamilisha mzunguuko wa 11.
Kwa maana hiyo Simba ina nafasi kubwa ya kujikita kileleni kwa kuongeza tofauti ya alama kati yake na Yanga kama itaifunga Lipuli.
Ligi kuu ya Vodacom ina ushindani mkali sana msimu huu ni muhimu kutofanya makosa kwani mbio za ubingwa sio za timu mbili kama ilivyozoeleka.
Singida United na Azam FC ni timu nyingine zinazoonekana kujipanga na zinaweza kuleta changamoto kwenye ubingwa

ADVERTISE HERE