Aussems lawamani vipigo vya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Feb 2019
Aussems lawamani vipigo vya Simba

Vipigo mfululizo vya mabao 5-0 katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika vimewasononesha mashabiki wa Simba ambao walikuwa na imani kubwa na timu yao msimu huu

Hii ni kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na mwekezaji wa klabu hiyo Bilionea Mohammed Dewji 'MO'.

Ni kweli wengi tuliamini Simba ilikuwa na nafasi ndogo ya kushinda michezo dhidi ya Vita Club na Al Ahly lakini tulikuwa na matumaini ya timu kufanya vizuri hasa baada ya kiwango kizuri walichoonyesha kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya JS Saoura

Lakini katika michezo miwili iliyopita mambo yamekuwa tofauti kabisa kinyume na matarajio ya wengi

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems hawezi kukwepa lawama za matokeo haya mabaya.

Kwenye mchezo dhidi ya Vita Club Simba Aussems alilaumiwa kwa kushindwa kutumia mbinu sahihi kupelekea Simba ikafungwa mabao 5-0

Jana tena dhidi ya Al Ahly, makosa yaleyale aliyofanya kwenye mchezo wa kwanza ameyarudia tena

Wakufunzi wengi wa soka hubadili mbinu kufuatana na uwezo wa wapinzani wao. Huwezi kutumia mfumo wa kushambulia ugenini unapocheza na timu kama Al Ahly

Simba sio timu ya kuruhusu mabao 10 katika michezo miwili.

Msimu uliopita Simba ilishiriki michuano ya Shirikisho idadi kubwa ya wachezaji ni hawahawa tofauti ni kocha tu

Ingawa haikufanikiwa kutinga hatua ya makundi lakini Simba ilitolewa kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya kulazimisha suluhu ya 0-0 dhidi ya Al Masry huko huko Misri

Naamini kama leo Simba ingekuwa bado chini ya Lechantre, kusingekuwa na hivi vipigo vya aibu. Lakini tunaheshimu uamuzi wa uongozi wa Simba kwa kuachana na kocha huyo ambaye gharama za kumhudumia zilikuwa kubwa kuliko uwezo wa klabu

Leo hii wengi wanajiuliza kwa nini kocha Aussems hataki msaidizi?

Wakati mwingine hutokea kocha akaishiwa mbinu lakini unapokuwa na msaidizi ataweza kukupa mawazo mbadala. Ndio maana Lechantre na Masudi Djuma walifanikiwa kwa sababu walishirikiana vizuri.

Lechantre alipotua Simba alimkuta Djuma akitumia mfumo wa 3-5-2 ambao ulikuwa ukiipa matokeo Simba. Lechantre hakuubadili ingawa alikuwa akifahamika yeye ni muumini wa 4-4-2

Ni vyema uongozi wa Simba ukashauriana na kocha Aussems juu ya umuhimu wa kuwa na kocha msaidizi ambaye atampa mawazo mbadala pale mambo yanapoharibika

Leo hii Simba inapofunwga au hata kuzidiwa huoni mabadiliko ya kiuchezaji, inaendelea kucheza hivyo hivyo

Kwa vipigo hivi, Aussems hawezi kukwepa lawama ingawa wachezaji nao wana sehemu yao ya lawana kwa kuwa ni wao waliokuwa dimbani.

Aidha matokeo haya yasiivuruge Simba, yatumike kusahihisha makosa yaliyoonekana.

Ikumbukwe bado Simba itachuana na timu hizo hapa jijini Dar es salaam kwenye dimba la Taifa

Nafasi ya kufanya vizuri nyumbani ipo, muhimu ni kwa benchi la ufundi kufanyia kazi mapungufu pamoja na kupokea ushauri wa wadau

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’