Tunawaheshimu Al Ahly lakini hatuwaogopi - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Feb 2019
Tunawaheshimu Al Ahly lakini hatuwaogopi - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanatambua mchezo wa leo dhidi ya Al Ahly hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa wapinzani wao ambao wamekuwa na mwendelezo mzuri katika kipindi cha miaka 10 iliyopita

Hata hivyo amesema Simba imejiandaa kikamilifu kuwapa Waarabu hao mtihani na kusisitiza kuwa hawakwenda Misri kutalii

"Tupo tayari kwa mchezo dhidi ya Al Ahly, nimewaambia wachezaji wangu tupo vitani tunacheza na timu bora yenye historia kubwa Afrika," Aussems alisema kwenye mkutano wa waandishi wa habari jana

"Tunawaheshimu wapinzani wetu lakini wasiwe na hofu yeyote, tunahitaji mapambano haswa kila moja ajitume na tunatakiwa tucheze soka la kasi na kushambulia mpira ni mbinu"

"Tinahitaji kupata matokeo mazuri ili kuwa na nafasi ya kusonga mbele kwenye hatua inayofuata ya michuano hii"

Naye kiungo Haruna Niyonzima ambaye akizungumza kwa niaba ya nahodha John Bocco, amesema hali za wachezaji ziko vizuri na hakuna majeruhi

Amesema uamuzi wa timu kuwahi kwenda Misri umekuwa na faida kwao kwani wameweza kuizoea hali ya hewa ya baridi kali

Jana jioni Simba ilifanya mazoezi ya mwisho kwenye dimba la Borg El Arab litakalotumika kwenye mtanange huo utakaopigwa leo saa nne usiku kwa saa za Tanzania

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’