Kamati ya Rufaa ya Maadili ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imetengua adhabu ya Meneja wa Simba Richard Robart iliyotolewa na Kamati ya Rufaa ya TFF.
Richard alifungiwa mwaka mmoja kujihusisha na mpira na faini ya Tsh. 4 Milioni.
Adhabu hiyo ilitolewa baada ya kutuhumiwa kuwa aliihujumu timu ya Taifa kwa kuchelewa kuwapa taarifa wachezaji wa Simba waliokuwa wanatakiwa kuingia kambini na kikosi cha Stars
ADVERTISE HERE