Inaelezwa kiungo mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya atajiunga na Pharco Fc inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Misri baada ya timu hiyo kumalizana na uongozi wa Simba
Kichuya huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Simba kitakachoikabili Al Ahly keshokutwa baada ya dili lake kuwa limekamilika
Aidha Pharco Fc iliyomsajili Kichuya itamtoa kwa mkopo kwenda klabu ya ENPPI SC inayoshiriki ligi kuu ya Misri
Mwanzoni mwa msimu Kichuya alisaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia Simba. Hata hivyo katika mkataba huo kulikuwa na kipengele kinachomruhusu kuondoka wakati wowote kama atapata timu nje ya nchi
ADVERTISE HERE