Kerr amtamani Tshabalala

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Nov 2017
Kerr amtamani Tshabalala
Beki wa kushoto wa Simba Mohamed Hussein 'Tshabalala' anawindwa na miamba ya soka nchini Kenya Gor Mahia, baada ya kocha wa timu hiyo Muingereza Dylan Kerr, kuonyesha kuvutiwa na kiwango cha nahodha huyo msaidizi wa vinara wa ligi kuu Tanzania Bara.

Aidha katika mahojiano na mtandao wa GOALTshabalala amesema kama inatokea nafasi hiyo yupo tayari kwasababu Gor Mahia ni klabu kubwa Afrika Mashariki na nifuraha kubwa miongoni mwa wachezaji wakigeni wanaochezea timu hiyo yenye historia na mafanikio makubwa nchini humo.

"Kwanini nikatae kwasababu mpira ndiyo kazi yangu na Gor Mahia ni timu kubwa yenye hadhi kama ya Simba, kwahiyo sioni sababu ya kugoma zaidi nitafurahi kwasababu nitakwenda kujiongezea ujuzi kwa kukutana na changamoto mpya kwenye ligi nyingine," amesema Tshabalala.

Beki huyo ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi ya Vodacom msimu uliopita amesema bado hajapata taarifa yoyote ya yeye kutakiwa na mabingwa hao wa Kenya, lakini endapo itazipata taarifa mapema atahakikisha anakwenda Nairobi kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo na taratibu nyingine za kujiunga na miamba hao wa kenya.

Kerr amewahi kuifundisha klabu ya Simba, na kwa bahati mbaya alitimuliwa baada ya mzunguko wa kwanza, kumalizika na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda Jackson Mayanja.

Kocha huyo amekuwa na mapenzi makubwa na wachezaji wa Tanzania na Afrika kwa ujuma kutokana na namna anavyofanya nao kazi kwa upendo.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’