Balozi wa Tanzania nchini Misri Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor ameupokea msafara wa kikosi cha Simba uliowasili nchini humo tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Jumamosi Februari 02, 2019
Hii ni mara ya pili kwa Meja Jenerali Issa kuipokea Simba nchini Misri.
Mwaka jana aliwapokea walipoenda kucheza na Al Masry kwenye mchezo wa marudiano wa kombe la Shirikisho hatua ya mtoano
Balozi huyo amewataka wachezaji wa Simba kuhakikisha wanajiandaa vizuri ili wapeperushe vyema bendera ya Tanzania kwa kushinda mchezo huo
Amesema nchini Misri sasa ni msimu wa baridi hivyo amewataka wachezaji wahakikishe wanajihifadhi ili baridi hiyo isije ikawaathiri kuelekea mchezo huo muhimu wa kundi D
Meja Jenerali Issa alizungumza na wachezaji mara baada ya timu kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cairo kabla ya kuanza safari kwenda mji wa Alexandria ambako ndipo watacheza mchezo dhidi ya Al Ahly.