Kikosi cha Simba kimeondoka leo kuelekea nchini Misri kuwakabili Al Ahly katika mchezo wa ligi ya mabingwa kundi D
Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Februari 02 2019
Wekundu hao wa Msimbazi wameondoka wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo.
Nahodha wa mabingwa hao wa Tanzania Bara John Bocco amesema wamejiandaa kupata matokeo yatakayo-waweze kupanda nafasi za juu katika kundi D
"Tunatambua hatua hii sio ya mtoano, tunaenda kucheza ugenini na pia kuna michezo tutacheza nyumbani. Tumejiandaa vizuri na tuna matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri," amesema Bocco
Haruna Niyonzima yeye amesema wanatambua mchezo huo hautakuwa mwepesi lakini kwa maandalizi waliyofanya, wataweza kuwadhibiti vinara hao wa kundi D
Kocha Patrick Aussems amesema vijana wake wako tayari kwa ajili ya mchezo wakitambua macho na dua za Watanzania wote ni kwao
Aidha Mkuu wa Msafari Crescentius Magori ambaye pia ni CEO wa Simba amesema walipata nafasi ya kuzungumza na wachezaji kuwaweka sawa kisaikolojia, hivyo anaamini watafanya kile walichoagizwa