Rweyemamu kupambana na utovu wa nidhamu Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Jan 2019
Rweyemamu kupambana na utovu wa nidhamu Simba

Baada ya tukio la baadhi ya wachezaji Simba kudaiwa kutoroka kambini usiku na kwenda 'kujirusha' siku moja kabla ya mchezo wa michuano ya SportPesa Cup dhidi ya Bandari Fc, jana Simba imetangaza kumteua Patrick Rweyemamu kuwa Meneja wa timu hiyo

Nafasi hiyo ilikuwa ikikaimiwa na Abbasi Ally tangu TFF ilipomfungia mwaka mmoja aliyekuwa Meneja wa timu hiyo Robert Richard

Mbali na majukumu mengine, Rweyemamu amepewa kazi maalum ya kuhakikisha anarejesha nidhamu ya baadhi ya wachezaji katika mstari

Rweyemamu aliye na taaluma ya ukocha, sio mgeni katika klabu ya Simba.

Aliwahi kuwa Meneja wa kikosi cha Vijana cha Simba kilichotoa nyota wengi wakiwamo Jonas Mkude, Ibrahim Ajib, Said Ndemla, Marcel Kaheza na wengineo wengi

Rweyemamu ametangulia nchini Misri na baadhi ya viongozi kuweka maandalizi kwa ajili ya mapokezi ya kikosi cha Simba nchini humo.

Simba inaondoka leo jioni kwenda Misri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’