Kibadeni ataka mabao zaidi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Nov 2017
Kibadeni ataka mabao zaidi Simba
Kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibaden amewaambia wachezaji wa timu hiyo, kuhakikisha wanafunga mabao mengi mchezo dhidi ya Lipuli, ili wazidi kuwaacha mbali wapinzani wao Yanga.

Lipuli ipo chini ya makocha Amri Said na Seleman Matola ambao ni wanachama hai na wachezaji wa zamani wa Simba kesho Jumapili watakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru kuwavaa vinara wa ligi hiyo Simba.

Kitendo cha Yanga kuwafunga Mbeya City mabao 5-0, alisema kiwe ishara kwao kujua kasi ya wapinzani wao inavyoweza kuwavunja nguvu itakapofikia hatua ya kupishana pointi moja moja.

"Wasipunguze kasi ya mabao, kila mechi angalau wafunge bao tatu, zinaweza kuwasaidia kulingana na msimamo wa ligi ulivyo mgumu,hilo ndilo linalowafanya wawe juu ya Azam,"

"Ni kweli kila timu imejipanga kwa ushindani, lakini Simba ina wachezaji wazoefu ambao wanaweza kuamua mechi,hao wanatakiwa kujua majukumu yao bila ya kusukumwa sukumwa,"alisema

"Ustaa unakuwa hauna maana endapo timu inakuwa na matokeo yasiyoridhisha, lakini inapendeza zaidi timu inapofanikiwa ikiwa chini ya mastaa,hivyo wajue wajibu wao ndipo Simba inaweza kuwa na jipya msimu huu,"alisema.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’