Simba yathibitisha uteuzi wa Meneja mpya, kwenda Misri Jumanne

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jan 2019
Simba yathibitisha uteuzi wa Meneja mpya, kwenda Misri Jumanne

Uongozi wa klabu ya Simba umethibitisha uteuzi wa Meneja mpya wa klabu hiyo Patrick Rweyemamu huku Abbas Ally aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo akirejeshwa katika majukumu yake ya awali ya uratibu wa timu

Katika hatua nyingine, kikosi cha Simba kitaondoka kesho Jumanne, Januari 29 2019 kuelekea nchini Misri kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa

Wachezaji 20 na viongozi wakiwemo wa benchi la Ufundi wataondoka kesho jioni

"Uongozi wa klabu ya Simba katika kuogeza ufanisi wa timu umemteua Ndg. Patrick Rweymamu kuwa meneja wa muda wa timu ya Simba, huku Ndg. Abbas Ally akiendelea na majukumu yake ya awali ya kuwa mratibu wa timu, imesema taarifa ya Simba

"Wakati huohuo kikosi cha wachezaji ishirini (20) na benchi la ufundi wakiambatana na viongozi kadhaa wataondoka kesho jioni January 29, 2019 kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kucheza mchezo wa hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya klabu ya Al Ahly.

"Simba itaondoka kwa shirika la ndege la Ethiopia kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia na kisha kuelekea mjini Alexandria, Misri ambapo mchezo huo unatarajia kuchezwa siku ya Jumamosi February 2, 2019"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’