Manara azindua Taasisi, Pafyum

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jan 2019
Manara azindua Taasisi, Pafyum

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara jana ilikuwa siku maalum kwake baada ya kuzindua Taasisi ya kuwasaidia watu wenye ulemavu wa ngozi inayofahamika kwa jina la Haji Manara Foundation na pia kuzindua pafyum inayofahamika kwa jina la De La Boss

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Serikali, waandishi wa habari, mashabiki na wachezaji na wawakilishi wa makundi mbalimbali

Hafla hiyo ambayo nusura imuingize Manara katika mgogoro na baadhi ya mashabiki wa Simba , ilifana sana

Manara amemshukuru Mwenye ez Mungu kwa kumuwezesha kufanikisha tukio hilo la kihistoria katika maisha yake

Amewaasa wale wote wanaotafuta mafanikio wasichoke kwani hakuna linaloshindikana chini ya jua

"Chini ya hili jua kila kitu kinawezekana,ni kuwa na dhamira,kujipanga,kuwa na nia njema na moyo mpana,lakini kubwa kujiweka na Mungu," amesema

Awashukia wanaomchonganisha na Simba

Katika hatua nyingine Manara amesema lipo kundi la watu linapotosha kile alichozungumza siku chache zilizopita kuwa aliwatukana mashabiki wa Simba

Manara amesema baada ya Simba kufungwa na Bandari Fc kuna shabiki alimtukana matusi makubwa na ndio huyo alikuwa akipambana nae

"Mimi siwezi na sijawaita Mashabiki wa Simba ni wapumbavu", amesema Manara

"Nimetaja neno pumbavu kwa mtu aliyenitukania mama yangu matusi mazito yasioandikika.

"Msilishwe matango pori na watu wenye chuki na hasadi, ninatoa Milioni tano kwa mtu yoyote atakaeisambaza clip inayoonyesha mm nimesemema Washabiki wa Simba wapumbavu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’