Aussems atahadharisha kuhusu waamuzi Misri

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jan 2019
Aussems atahadharisha kuhusu waamuzi Misri

Baada ya kumalizika kwa michuano ya SportPesa Cup, Simba ikifanikiwa kumaliza nafasi ya tatu, mabingwa hao watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara wanajiandaa na safari ya kuelekea nchini Misri kuwakabili mabingwa wenzao Al Ahly katika mchezo wa ligi ya mabingwa, kundi D

Simba itachuana na Al Ahly Februari 02

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema licha ya kufanya maandalizi ya kimchezo, wanajiandaa 'kisaikolojia' kukabiliana na maamuzi ya 'hovyo' kutoka kwa waamuzi watakao-chezesha mchezo huo

Aussems amesema ni kawaida kwa timu zinazokwenda kucheza Misri katika michuano ya vilabu barani Afrika kukumbana na changamoto hiyo

AS Vita ilipokwenda Misri ililazwa mabao 2-0 katika mchezo ambao mlinzi wa timu hiyo, Charles Kalonji alipewa kadi nyekundu tata mapema tu kwenye kipindi cha kwanza

"Tunatakiwa kuwa sawa kisaikolojia. Siku zote unapocheza na timu kama Al Ahly unatakiwa kutambua kuwa kabla ya mchezo kuanza wao wanakuwa mbele kwa bao moja," amesema Aussems

"Hapa namaanisha mpira ukianza akili yetu inatakiwa kuanza kutafuta bao la kusawazisha kwani lazima watapewa motisha na waamuzi"

Simba inahitaji alama moja kutoka michezo yake miwili ya ugenini huku ikihakikisha inashinda michezo yote miwili ya nyumbani kujiwekea mazingira ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’