Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ametumia vikosi tofauti katika michuano ya kombe la Mapinduzi na SportPesa Super Cup.
Uamuzi huo uliwakwaza baadhi ya mashabiki hasa ikizingatiwa wengi walitamani kuona Simba inatwaa mataji hayo
Lakini Aussems amesema uamuzi huo ulikuwa ni lazima kwani Simba inakabiliwa na mashindano muhimu zaidi
"Michuano ya kombe la Mapinduzi na hii ya Sportpesa haikuwa kipaumbele changu kwa kuwa haikupeleki kushiriki michuano ya CAF", amesema Aussems
"Malengo yetu ilikuwa kutinga hatua ya Makundi, tumefanikiwa na bado tuna michezo ya ligi ya mabingwa".
"Nililazimika kubadilisha wachezaji kwa usalama zaidi kwani ndani ya siku sita unacheza michezo mitatu tungeweza kupata majeruhi zaidi"
"Tutapambana kwenye ligi tupate alama zitakazotuwezesha kushiriki ligi ya mabingwa msimu ujao, hayo mengine hayakuwa malengo yangu"
Mkataba wa Aussems ulimtaka kuhakikisha Simba inatinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa na pia kuhakikisha Simba inatetea ubingwa wake
Tayari amefanikiwa kuipeleka Simba hatua ya makundi na sasa amebaki na jukumu la kuhakikisha Simba inatetea ubingwa wake iliyotwaa msimu uliopita