Kariobang Sharks imeichapa Bandari Fc bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali na kutwaa taji la SportPesa Cup
Taji hilo limeelekea nchini Kenya kwa msimu wa tatu mfululizo
Mapema Simba ilijihakikishia nafasi ya tatu baada ya kuifunga Mbao Fc kwa mikwaju ya penati 5-3 kufuatia matokeo ya suluhu ya bila kufungana
K. Sharks imetwaa kitita cha dola 30,000 na imepata tiketi ya kuchuana na Everton mwezi Julai katika mchezo utakaopigwa nchini Kenya
Kwa mara nyingine tena, timu za Tanzania zimeshindwa 'kujitutumua' dhidi ya Wakenya zikiendelea kuwa wasindikizaji katika michuano hiyo
ADVERTISE HERE