Beki Lamine Moro amecheza michezo yote mitatu ya Simba katika michuano ya SportPesa Cup na ana nafasi kubwa ya kusajiliwa baada ya kuonyesha kiwango kizuri
Lamine raia wa Ghana alikuja Simba kufanya majaribio akitokea klabu ya BuildCon ya Zambia

Naye mshambuliaji Sadney Urikhob raia wa Namibia aliyecheza michezo miwili kati ya mitatu huenda akasajiliwa baada ya kuonyesha kiwango kizuri
Licha ya kutofunga hasa katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Mbao Fc, Sadney ameonyesha ni mshambuliaji mzuri, anajua kutengeneza nafasi na pia ameonyesha kuwa ni mshambuliaji anayeweza kusababisha madhara kwa timu pinzani wakati wowote anapokuwa na mpira
Kocha Patrick Aussems amemsifia mshambuliaji huyo kuwa ana uwezo na alikuwa akimfuatilia hata kabla hajatua Simba
Mtogo Kissimbo Ayi-Abel yeye ameshindwa kuonyesha makali yake. Ni dhahiri atakuwa ameshindwa majaribio