Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema amekuwa akipokea meseji za matusi, kejeli na vitisho kutoka kwa mashabiki baada ya Simba kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la SportPesa hapo jana kwa kufungwa mabao 2-1 na Bandari Fc
Manara amesema baadhi ya mashabiki wamekwenda mbali zaidi kwa kumtaka aahirishe tukio la kusherehekea siku yake ya kuzaliwa linalokwenda sambamba na uzinduzi wa 'perfume' yake
Manara amewataka mashabiki hao waelewe kuwa matukio atakayoyafanya Januari 27 ni ya kwake binafsi na sio ya klabu ya Simba
"Kiukweli sijapenda hili linaloendelea mitandaoni toka jana," ameandika Manara kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram
"Kuna watu wanaotukana na kusema ni lazma nihairishe Event yangu ya kesho kisa Simba imefungwa!! HAPANA..
"Vitu vingine haviwezi kusimama kisa Simba imeloose game,na hasa kama jambo lenyew ni la msingi sana
"Unaachaje jambo linalokwenda kusaidia watu kama la taasisi yangu kisa matokeo ya uwanjani?
"Naachaje kuzindua Perfume yangu itakayosaidia kimapato jamii yangu,mimi na Taifa langu kwa kulipa kodi kisa mpira?
"Ninaitumikia Simba kwa moyo mmoja na nnajitoa kupitiliza kisha nnatukanwa kupita mtu yoyote katika medani ya Soka na sijali ili mradi Simba yangu ifanikiwe,halafu eti nihairishe mambo yangu binafsi kisa tumefungwa?
"Birthday yangu ni Jan 18 nilihairisha kila kitu kupisha majukumu tulionayo na nikaipanga kesho!!
Why nihairishe!
"Guys sihairishi Na Haji Manara foundation,De la boss Perfume zote zitazinduliwa kesho!!"