Kiungo tegemeo wa kikosi cha Al Ahly Walid Soliman amepata majeraha ya goti ambayo yatamuweka nje kwa wiki tano
Kiungo huyo atakosa michezo yote miwili ya ligi ya mabingwa dhidi ya Simba
Klabu ya Al Ahly inayoongoza kundi D, imethibitisha kuwa kiungo huyo atakuwa nje kwa wiki tano akiuguza majeraha hayo
Soliman ni 'engine' ya kikosi cha Al Ahly akiwa ndiye mchezeshaji wa timu hiyo
Simba itachuana na Al Ahly Februari 02 nchini Misri kabla ya timu hizo kurudiana jijini Dar es salaam baada ya siku 10 katika mchezo wa nne kundi D
ADVERTISE HERE