Vurugu zilizofanywa na mashabiki wa Ismaily ya Misri kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Club Africain zimeiponza timu hiyo baada ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) kuiondosha katika michuano ya ligi ya mabingwa
Mashabiki wa Ismaily walimrushia mawe na chupa mshika kibendera ambapo katika dakika ya 86 mwamuzi alimaliza mchezo baada ya vurugu kushamiri
Kulingana na taarifa iliyotolewa na CAF, mashabiki wa timu hiyo walimrushia mawe mchezaji wa Club Africain aliyekuwa anataka kupiga kona na kupelekea mwamuzi kusimamisha pambano
Kundi C sasa limebaki na timu tatu CS Contantinos, Club Africain na TP Mazembe
CS Constantinos ndio vinara wa kundi hilo wakijikusanyia alama sita wakati Club Africain na Mazembe hazina pointi kwa kuwa alama walizopata dhidi ya Ismaily zimefutwa
