Katika mchezo wa leo dhidi ya AFC Leopards kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems aliwatumia wachezaji wawili wanaofanya majaribio beki Lamine Moro na mshambuliaji Hunlede Kisimbo
Klabu ya AFC Leopards imemuwekea pingamizi Lamine raia wa Ghana kutokana na leseni yake kuonekana ni mchezaji halali ya wa Buildcon FC ya Zambia.
Saol Shikuku mjumbe wa kamati ya utendaji ya AFC Leopards amesema kanuni za mashindano ya Sportpesa zinataka wachezaji watakaotumika lazima wawe na leseni kutoka Shirikisho la mpira ya nchi ambazo vilabu vinatokea.
Lamine alionyesha kiwango kizuri kwenye mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Cup
Licha ya kuwepo kanuni hiyo iliyotumiwa na AFC Leopards kupinga Simba kumtumia Lamine, ipo kanuni nyingine ambayo inaruhusu timu kutumia mpaka wachezaji watatu ambao wamepatiwa Leseni za mda na chama cha soka cha nchi husika ambayo mchezaji anacheza