Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amewapongeza wachezaji wa timu hiyo kwa kufanikiwa kutinga nusu fainali ya michuano ya SportPesa Cup baada ya kuilaza AFC Leopards mabao 2-1
Aussems amesema leo Simba ilitengeneza nafasi nyingi lakini kukosekana kwa umakini kuliwanyima ushindi mnono mabingwa hao wa Tanzania Bara
"Tumetengeneza nafasi nyingi lakini tumetumia mbili tu. Nimeyaona mapungufu, nitayafanyia kazi kuhakikisha tunatumia vyema nafasi tunazopata," amesema Aussems
"Kwa ujumla tumecheza vizuri sana lakini sikufurahishwa na makosa tuliyofanya yaliyopelekea Leopards kupata bao"
Simba itachuana na Bandari Fc kwenye mchezo wa nusu fainali utakaopigwa keshokutwa Ijumaa saa nane mchana wakati mchezo mwingine wa nusu fainali utakuwa kati ya Mbao Fc dhidi ya K. Sharks
Simba ina nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa wa michuano ya SportPesa mwaka huu