Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema timu yake inakabiliwa na ratiba ngumu kutokana na kushiriki michuano mbalimbali.
Kikosi cha mabingwa hao wa Tanzania Bara leo kinashuka katika dimba la Taifa kuikabili AFC Leopards kwenye mchezo wa robo fainali michuano ya SportPesa Cup
Baada ya michuano hiyo kumalizika Januari 27, Simba itaelekea nchini Misri kuikabili Al Ahly kwenye mchezo wa mzunguuko wa tatu wa ligi ya mabingwa kundi D.
Mchezo huo utapigwa Februari 02
"Michuano hii ya SportPesa tunaruhusiwa kutumia wachezaji 22 na pia tumepewa ruhusa kutumia wachezaji watatu walio kwenye majaribio hivyo tutawajumuisha kwenye kikosi wachezaji tunaowajaribu," amesema Aussems
"Tunakabiliwa na ratiba ngumu. Angalia kwenye ligi sisi tumecheza michezo 14 lakini timu nyingine zimecheza hadi michezo 22, kuna tofauti ya michezo nane, hii ni hatari"
"Najua TFF watatupangia ratiba ya kucheza michezo hiyo katika muda mfupi mfupi huku wakati huo tukiwa tunakabiliwa na michuano ya ligi ya mabingwa"
"Lakini hatutakuwa na namna ni lazima tucheze"
Katika mchezo wa leo Simba ikawakosa baadhi ya wachezaji wake wanaosumbuliwa na majeruhi
Miongoni mwa wachezaji hao ambao kocha Aussems amethibitisha kuwa hawatakuwa sehemu ya kikosi cha wachezaji 22 wanaoshiriki michuano hiyo ni pamoja na Asante Kwasi, Yusufu Mlipili na Adam Salamba
Aidha Shomari Kapombe na Erasto Nyoni nao wanaendelea na matibabu ya majeraha yao