Kocha Mkuu wa Simba Joseph Omog tayari amewasilisha mapendekezo yake kwa Kamati ya Usajili inayoongozwa na Zacharia Hans Poppe.
Katika mapendekezo hayo, Omog amewataka viongozi hao wamuongezee wachezaji watatu kwenye kikosi chake wakati huu wa usajili wa dirisha dogo.
Kipa, Beki wa Kati na Winga ndio nafasi tatu ambazo kocha ametaka ziimarishwe huku kocha msaidizi Masudi Djuma akipendekezwa kusajiliwa kwa mshambuliaji.
Kipa Said Mohammed 'Nduda' huenda asirejee dimbani hadi msimu ujao baada ya kufanyiwa upasuaji nchini India miezi michache iliyopita.
Aidha majeruhi ya mara kwa mara yanayowakabili nahodha Method Mwanjali na Salim Mbonde pia yamepelekea benchi la Ufundi kuhitaji kusajiliwa beki mwingine wa kati.
Pendekezo la kusajiliwa kwa winga ni ili aje asaidiane na Shiza Kichuya ambaye amecheza michezo mingi kwa kuwa hana msaidizi kwenye nafasi yake.
Kocha Msaidizi Djuma amependekeza kusajiliwa kwa mshambuliaji wa Rayon Sport Shasir Nahima huku kukiwa na uwezekano wa mshambuliaji Laudirt Mavugo kutolewa kwa mkopo.
Wachezaji wengine wanaotajwa kuwa kwenye rada za Simba ni Salum Kabunda, mlinda lango Deo Munishi 'Dida'.
Pia Simba huenda ikajaribu kumrejesha beki wake mkongwe Kelvin Yondani ambaye kwa sasa anafanya vizuri kwenye klabu ya Yanga.
Imeelezwa mkataba wa Yondani unaelekea kumalizika mwezi ujao.

ADVERTISE HERE