Walinzi Asante Kwasi na Yusufu Mlipili hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba cha wachezaji 22 watakaoshiriki michuano ya SportPesa Cup iliyoanza leo jijini Dar es salaam
Kwasi alipewa ruhusa ya kwenda kwao Ghana kutokana na matatizo ya kifamilia wakati Mlipili ameshindwa kujumuishwa kutokana na uamuzi wa kocha Patrick Aussems
Wachezaji wengine ambao watakosa michuano hiyo kutokana na majeruhi ni pamoja nahodha John Bocco, Shomari Kapombe na Erasto Nyoni
Simba inatarajiwa kucheza na AFC Leopards kesho Jumatano ukiwa ni mchezo wake wa kwanza tangu iliporejea kutoka Congo
Aussems anatarajiwa kutumia wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ili kuhakikisha mabingwa hao wa Tanzania Bara wanatwaa taji la michuano hiyo.
Simba pia itatumia michuano hiyo kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly utakaopigwa ugenini Februari 02 2019