AFC Leopards ijiandae 'kisaikolojia' kumkabili Simba aliyejeruhiwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jan 2019
AFC Leopards ijiandae 'kisaikolojia' kumkabili Simba aliyejeruhiwa

Michuano ya SportPesa Super Cup inaanza leo lakini mabingwa wa Tanzania Bara Simba wao watashuka dimbani kesho Jumatano kuikabili AFC Leopards

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amepania kutumia michuano hii kukiandaa kikosi chake kinachotarajiwa kwenda nchini Misri punde baada ya michuano kumalizika Januari 27 kuikabili Al Ahy

Baada ya kurejea kutoka Congo usiku wa kuamkia jana, moja kwa moja kikosi cha Simba kilielekea kambini kujiwinda na mchezo wa kesho

Baada ya kufungwa mabao 5-0 na Vita Club juzi, Simba inahitaji kurudisha imani ya mashabiki wake kwa kushinda mchezo wa kesho na kikubwa zaidi ni kuhakikisha ubingwa wa michuano hiyo unakwenda Msimbazi

Ni mchezo ambao Simba haitakuwa na masihara, bila shaka Aussems atashusha 'full mziki' kuikabili AFC Leopards inayoshika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Kenya

Simba inahitaji ushindi katika mchezo huo kwani matokeo tofauti na ushindi yatashusha morali ya wachezaji na hata mashabiki ambao wamekuwa chachu ya mafanikio ya mabingwa hao kutokana na sapoti wanayotoa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’