Wachezaji wapya Simba kujaribiwa michuano ya SPortPesa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Jan 2019
Wachezaji wapya Simba kujaribiwa michuano ya SPortPesa

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi Klabu ya Simba, imeshusha majembe mawili ya maana huku lingine likitarajiwa kuingia muda wowote kuanzia sasa.

Wakali hao wamekuja kufanya majaribio ili waweze kuichezea timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Wachezaji hao ni beki wa kati, Mghana Moro Lamine na straika Mtogo Hunlede Kissimbo Ayi walianza kufanya mazoezi na Simba jana Jumatatu jioni katika Uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es Salaam chini ya uangalizi wa Kocha Patrick Aussems ambaye ndiye atakayetoa kauli ya mwisho juu ya usajili wao wapewe mikataba au wafyekelewe mbali.

Si hao tu, mabosi wa Simba katika kuhakikisha wanaimarisha kikosi chao zaidi, straika mwingine kutoka nchini Namibia anatarajiwa kuingia muda wowote kuanzia sasa kwa ajili ya majaribio kama hayo.

"Hawa wachezaji tumewaleta kwa ajili ya majaribio na si hawa wawili tu bali watakuwa watatu na mwingine straika kutoka Namibia mtamuona siku si nyingi atawasili nchini," alisema mmoja wa kigogo wa Simba ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi.

"Tutawatumia wachezaji hawa katika mashindano ya SportPesa na itakuwa kama sehemu yao ya majaribio ili kuona kama wanauwezo wa kuisaidia Simba ili tuwasajili na kama watakuwa hawana uwezo kwa mujibu wa kocha wetu tutaachana nao," alisema.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’