Bakisheni ubingwa wa SportPesa nyumbani - Tarimba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Jan 2019
Bakisheni ubingwa wa SportPesa nyumbani - Tarimba

Mkurugenzi wa utawala na udhibiti wa SportPesa Abbasi Tarimba amezitaka timu zinazoshiriki michuano hiyo kutoka hapa Tanzania kuhakikisha mwaka huu zinabakisha ubingwa hapa nchini.

Michuano ya SportPesa Super Cup inaingia msimu wa tatu kesho kwa michezo miwili kupigwa kwenye dimba la Taifa

Mchezo wa kwanza unaotarajiwa kuanza saa nane utakuwa kati ya Singida United dhidi ya Bandari Fc kisha kufuatiwa na mchezo wa Yanga dhidi ya K Sharks

Keshokutwa Jumatano kutakuwa na michezo mingine miwili ambapo mchezo wa mapema saa nane ni kati ya Mbao Fc dhidi ya Gor Mahia na utafuatiwa na mchezo kati ya Simba dhidi ya AFC Leopards

Katika msimu wake wa kwanza michuano hiyo ilifanyika hapa Tanzania na Gor Mahia ikaibuka washindi na wakashinda tena michuano hiyo ilipofanyika nchini Kenya mwaka jana katika msimu wa pili

Tarimba amesema timu za Tanzania hazipaswi kuipuuzia michuano hiyo kwa kutumia vikosi vya pili wakati wenzao Wakenya wanafahamu umuhimu wake

"Haiwezekani tena safari hii ubingwa wa michuano hii ukaenda Kenya kama ilivyofanyika miaka miwili iliyopita. Ni lazima timu za nchini kupambana kuhakikisha wanaubakisha ubingwa hapa nchini," amesema Tarimba kwenye Mkutano na Waandishi wa habari leo

"Tayari nimekutana na viongozi wa Simba, Yanga, Mbao FC na Singida Utd nikiwasisitizia ubingwa ubaki nyumbani.

"Nimewaambia waache mzaha kabisa kwa kutumia wachezaji wa vikosi vya pili na badala yake kuwatumia wale wa kikosi cha kwanza.

"Mara kadhaa tumeziona Simba na Yanga zikitumia wachezaji wa kikosi cha pili, hivyo mwaka huu hatutaki kitu hicho kitokee kikubwa tunataka ubingwa"

Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha Mil 70 pamoja na kukata tiketi ya kuchuana na Everton Fc inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’