Kampuni ya SportPesa iliyoandaa michuano ya SPortPesa Super Cup imetaja viingilio vya michuano hiyo inayoanza kesho Jumanne, Januari 22 na kumalizikia Januari 27
Viingilio vya michuano hiyo ambayo pia itarushwa mbashara na DSTV (SS9), vimefanywa rahisi ili kuwapa nafasi mashabiki wengi wa soka kuishuhudia michuano hiyo itakayopigwa dimba la Taifa.
VIP A ni Tsh 10,000/-, VIP B na C ni Tsh 5,000/- wakati upande wa Mzunguuko ni Tsh 2,000/-
Simba ni miongoni mwa timu nane zinazoshiriki michuano hiyo ambapo itashuka dimbani keshokutwa Jumatano kuikabili AFC Leopards
Timu nyingine zinazoshiriki michuano hiyo ni Gor Mahia, KK Sharks, Bandari Fc, Mbao Fc, Singida United na Yanga
ADVERTISE HERE