Juzi kwenye mchezo dhidi ya Vita Club Simba ilivaa jezi zisizo na nembo yoyote sababu imetajwa ni timu hiyo kuzuiwa na Shirikisho la soka soka barani Afrika (CAF) kuvaa jezi zenye nembo ya mdhamini wao kampuni ya SportPesa
Katika mchezo huo Simba ililazimika kufanya maarifa ya haraka ili kupata jezi zisizo na nembo ili kukidhi matakwa ya waandaaji wa michuano hiyo ambayo imebainika kuwa kampuni ya 1XBet ni miongoni mwa wadhamini wake
1XBet ina ushindani wa kibiashara na SportPesa
Hii sio mara ya kwanza kwa timu za Tanzania kuzuiwa kutumia jezi zenye nembo ya mdhamini.
Mwaka jana Yanga iliyokuwa ikishiriki michuano ya Shirikisho ilizuiwa kutumia jezi zenye nembo ya SportPesa pia
ADVERTISE HERE