Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba watashiriki michuano ya SportPesa Super Cup inayotarajiwa kuanza keshokutwa uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Simba ni miongoni wa timu nane zinazoshiriki michuano hiyo iliyoingia msimu wa tatu mwaka huu
Simba ambayo ilitinga fainali za michuano ya awamu iliyopita, itacheza na AFC Leopards siku ya Jumatano, Januari 23 2019
Uongozi wa timu hiyo umeahidi kutumia kikosi chake cha kwanza kuhakikisha wanatwaa ubingwa walioukosa mwaka jana kwa kufungwa na Gor Mahia mabao 2-0 kwenye mchezo wa fainali
Kikosi cha Simba kinaondoka nchini Congo leo ambako jana kilicheza na AS Vital Club katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliomalizika kwa wenyeji kushinda mabao 5-0
Timu zinazoshiriki michuano hiyo mwaka huu ni Simba, Yanga, Singida United na Mbao Fc kutoka Tanzania wakati kutokea nchini Kenya ni Gor Mahia, K. Sharks, AFC Leopards na Bandari Fc
Bingwa wa michuano hiyo atanyakua kombe na fedha taslimu dola 30,000 (Mil 70) pia kukata tiketi ya kucheza na Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza