Tusikate tamaa bado tuna nafasi - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Jan 2019
Tusikate tamaa bado tuna nafasi - Manara

Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kipigo cha mabao 5-0 ilichopokea Simba kutoka klabu ya Vita jana ni matokeo mabaya sana lakini Wana Msimbazi hawapaswi kukata tamaa

"Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa wenzetu wameyatumia kutuadhibu," amesema Manara

"Lakini hatupaswi kukata tamaa, tutajipanga ili tuweze kufanya vizuri michezo ijayo"

"Tuna michezo miwili nyumbani na mingine miwili ugenini. Tumepoteza pambano na sio vita"

Naye kocha Msaidizi wa AS Vital Club Raul Shungu ametaja sababu iliyoiponza Simba kwenye mchezo wa jana

Shungu aliyewahi kufanya kazi nchini katika klabu ya Yanga amesema aliiangalia Simba na kubaini ni nzuri lakini kilichowaponza jana ni kutokuwa na mpango mzuri wa kutengeneza mashambulizi

"Walikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira. Walipiga pasi nyingi zisizo na faida kwani hawakuwa wakisogea mbele. Pia walikuwa wakicheza taratibu sana",amesema

"Sisi tulipopata mpira tulitumia udhaifu wao kwa kupeleka mashambulizi ya kasi langoni kwao,"amesema

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ana kazi ya kufanya kabla timu hiyo kwenda nchini Misri kuikabili Al Ahly Februari 02 2019

Aussems anapaswa kurekebisha makosa ya safu ya ulinzi na sehemu ya kiungo ambayo haikuwa katika ubora wake katika mchezo wa jana

Aidha matokeo hayo ya ugenini yasiiondoe Simba mchezoni kwani katika michuano hii kila timu imejizatiti kushinda michezo yao ya nyumbani

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
46m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’