Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye dimba la Stade des Martyrs tayari kwa mchezo dhidi ya AS Vital Club
Mchezo huo utapigwa kesho Jumamosi, Januari 19 2019 saa moja usiku kwa saa za Tanzania katika uwanja huo unaobeba mashabiki 80,000
Mapema katika Mkutano wa waandishi wa habari, kocha wa Simba Patrick Aussems alisema wamejiandaa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo huo na hawatacheza kwa kujihami
Nae nahodha msaidizi wa Simba Haruna Niyonzima alisema watasaka ushindi wa ugenini lakini hata kama watapata matokeo ya sare hayatakuwa mabaya kwao
Simba iko kileleni mwa kundi D linalojumuisha pia Al Ahly, AS Vita Club na JS Saoura
Timu zitakazomaliza nafasi ya kwanza na ya pili katika kundi zitatinga robo fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi kwa ngazi ya vilabu