Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)TFF leo Ijumaa Januari 18,2019 limewatangaza Biko Sports kudhamini tuzo za mchezaji bora wa mwezi na kocha bora.
Biko Sports katika kipindi chote cha msimu wa 2018/2019 kilichobakia watatoa fedha kwa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora ambapo kila mmoja atapata shilingi milioni 1.
Mbali na fedha, Biko Sports watatoa tuzo kwa kocha na mchezaji bora wa kila mwezi.
TFF ina utaratibu wa kuwazawadia wachezaji bora na makocha wa kila mwezi pamoja na wale wa msimu mzima.
ADVERTISE HERE