Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kikosi chake hakikwenda Congo kujilinda bali kusaka ushindi katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya AS Vita Club utakaopigwa kesho Jumamosi.
Akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo, Aussems amesema anatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini hawatabadili aina yao ya uchezaji
"Itakuwa mechi ngumu lakini hatujaja hapa kuzuia, tumekuja hapa kujaribu kutengeneza nafasi kama ilivyo kwa michezo yetu mingine na kujaribu kufunga," amesema Aussems
Mchezo dhidi ya Vita utapigwa saa 11 jioni kwa saa za Congo ambapo kwa Tanzania itakuwa ni saa moja usiku
Leo JS Saoura itachuana na Al Ahly kwenye mchezo mwingine wa mzunguuko pili, kundi D
ADVERTISE HERE