Aussems atamba, vijana wameiva

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Jan 2019
Aussems atamba, vijana wameiva

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kikosi chake kina matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vital Club

Simba iko nchini Congo tangu jana ikiendelea na maandalizi ya mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini

Aussems amesema amevutiwa na mwitikio wa wachezaji wake katika mazoezi maalum anayowapa kuwakabili Wacongomani hao ambao wamekuwa wakifanya vizuri wanapocheza kwenye uwanja wao wa nyumbani

Amesema ushindi mnono waliopata kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya JS Saoura umeongeza utulivu kwa kikosi chake

"Tumejiandaa kikamilifu, vijana wangu wamepata maelekezo yote kwa ajili ya mchezo huo, na wako tayari"

"Tulishinda mchezo wa kwanza nyumbani, wapinzani wetu walifungwa. Tunajua watakuwa na presha ya kupata ushindi, tutacheza kwa tahadhari kubwa kuhakikisha tunafanya vizuri kwenye mchezo huo," amesema Aussems

Vinara hao wa kundi D walitua jana nchini Congo na jioni kujifua kwenye dimba la Stade des Martyrs ambapo mchezo huo utapigwa

Leo Simba itafanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja huo huo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
57m ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
16h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
19h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’