Nilianza kuishabikia Simba nikiwa na miaka minne - MO

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Jan 2019
Nilianza kuishabikia Simba nikiwa na miaka minne - MO

Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'MO' amekuwa mshabiki wa Simba kwa miaka mingi. Mwenyewe amesema alianza kuishabikia Simba akiwa na umri wa miaka minne.

Mo anasema amebahatika kuzaliwa katika familia ya Wana Msimbazi kwani kuanzia babu yake mpaka watoto wake wote ni mashabiki wa Simba

"Nilianza kuishabiki Simba nikiwa na umri wa miaka minne. Kipindi hicho hakuna TV tulikuwa tukisikiliza mpira kupitia redio"

"Mwaka 2003 nikiwa mdhamini wa Simba mafanikio tuliyoyapata ni kuwa timu ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati kuifunga klabu bingwa ya Afrika wakati huo Zamalek ya Misri. Na ushindi huo unabaki kuwa moja ya mafanikio makubwa katika historia ya klabu yetu."

"Lengo langu ni kuifanya Simba kuwa timu yenye mafanikio sio Tanzania tu na Afrika Mashariki, bali ukanda wote wa Afrika"

Tayari uwekezaji wake katika klabu ya Simba ndani ya misimu miwili umekuwa na mafanikio makubwa

Msimu uliopita Simba ilitwaa ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya kwanza baada ya kuukosa kwa misimu minne.

Msimu huu mafanikio yamekuwa makubwa zaidi baada ya kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa

Simba imedhamiria kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
2h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
7h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
22h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
2d ago
READ MORE β†’