Maxime aipongeza Simba, atoa angalizo kuhusu viporo TPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Jan 2019
Maxime aipongeza Simba, atoa angalizo kuhusu viporo TPL

Huku wakiwa wanakabiliwa na mechi za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya makundi, mabingwa watetezi wa Ligi Kuu wametakiwa kutokubali kuwa na idadi "kubwa ya viporo" vya ligi hiyo ya juu Tanzania Bara.

Simba iko Kundi D ikiwa na JS Saoura ya Algeria, Al Ahly (Misri) na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime ameitaka Simba isikubali kurundikiwa michezo ya viporo kwani endapo wataendelea kubaki nyuma, watawapa mwanya wapinzani wao kuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu.

Maxime alisema kuwa kucheza mechi katikati, zitaisaidia Simba kujiweka imara kama ilivyokubali kucheza baadhi ya michezo katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi karibuni huko Zanzibar.

"Kwa maoni yangu, Simba inajiweka katika nafasi mbaya, tofauti ya mechi zake na timu nyingine ni kubwa, lakini kiufundi haitawasaidia kukaa bila kucheza mechi za ushindani," alisema beki huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Aliongeza kuwa Simba inatakiwa kuacha woga, icheze mechi za Ligi Kuu Bara na vile vile za Ligi ya Mabingwa Afrika ili kuonyesha kwamba wako tayari katika mapambano.

Hata hivyo, Maxime aliwapongeza wachezaji wa Simba kwa hatua waliyofika na kuwakumbusha kutobweteka kwa sababu bado wana safari ndefu.

Kikosi cha Simba kinatarajia kuondoka nchini leo asubuhi kuelekea Kinshasa ili kuwavaa wenyeji AS Vita katika mchezo wa pili wa Kundi D utakaochezwa Jumamosi.

Nipashe

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’