Akina dada wa Simba Queens leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya Wanawake baada ya kuchapwa bao 1-0 na JKT Queens
Kabla ya mchezo huo Simba Queens inayoshika nafasi ya pili, ilikuwa imeshuka dimbani mara tano, ikishinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja.
JKT Queens imejipambanua kuwa timu bora katika michuano hiyo ikiwa imeshinda michezo yake yote sita. Ni Simba Queens pekee ambao imefungwa bao 1 na JKT Queens.
Wakina dada hao wamekuwa wakigawa vipigo hadi vya bao 16-0 katika ligi hiyo
Watani zao Yanga Princess wameendelea kugawa pointi kwenye ligi hiyo baada ya leo kulazwa mabao 4-1 na Baobab Queens iliyokuwa inashika mkia kabla ya mchezo huo
ADVERTISE HERE