Bodi ya ligi yatembeza adhabu VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Nov 2017
Bodi ya ligi yatembeza adhabu VPL
Kamati ya Bodi ya Ligi Kuu ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi katika kikao chake cha Novemba 22, 2017 ilipitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi kwa msimu wa 2017/2018 inayoendelea hivi sasa.

Klabu ya Tanzania Prisons imepewa onyo kali kwa kuwakilishwa kwenye benchi na ofisa tofauti na yule aliyeudhuria kikao cha maandalizi (pre match meeting) cha mchezo kati yake na Kagera Sugar uliofanyika Novemba 4, 2017 kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Katika kikao hicho, Prisons iliwakilishwa na Meneja wake Erasto J. Ntabah lakini kwenye benchi alikaa Hassan Mtege. Adhabu ya Onyo Kali kwa klabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Pia, Erasto J. Ntabah amesimamishwa hadi suala lake la kutoka jukwaani na kwenda kumfokea Mwamuzi wa Akiba litakaposikilizwa na Kamati ya Nidhamu ya TFF. Amesimamishwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu kuhusu Usimamizi wa Ligi.

Mchezaji Benjamin Asukile wa Tanzania Prisons amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu na Mwamuzi kwa kosa la kumpiga kiwiko kwenye paji la uso mchezaji wa Kagera Sugar.

Kocha wa Azam FC, Aristica Cioaba amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kuwafuata waamuzi na kuwalalamikia kwa kurusha mikono akionyesha kutoridhika na maamuzi yao.

Alifanya hivyo kwenye mechi namba 69 ya Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Ruvu Shooting iliyofanyika Novemba 4, 2017 kwenye Uwanja wa Azam Complex na adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 40(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Makocha.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’