Baada ya kuwafumua watani zao wa jadi Yanga Princess mabao 7-0 wakina dada wa Simba Queens leo wanashuka tena dimba la Karume kuwakabili kina dada wa JKT Queens
Kiingilio cha mchezo huo ni Shilingi 2000 tu.
JKT Queens ndio vinara wa ligi kuu ya Wanawake wakiwa wameshinda michezo yao yote mitano na kufunga mabao zaidi ya 40
Simba Queens inashika nafasi ya pili ikiwa imeshinda michezo minne na kutoka sare mchezo mmoja na kujikusanyia alama 13
Mchezo huo sio wa kukosa kwani utakuwa 'derby' ya vinara wa ligi kuu ya Wanawake
ADVERTISE HERE