Salamba afafanua tuhuma za kushuka kiwango

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jan 2019
Salamba afafanua tuhuma za kushuka kiwango

Mshambuliaji Adam Salamba ambaye anatabiriwa kuja kuwa mmoja wa wachezaji tegemeo kwa Taifa, amewataka mashabiki Simba wasimlaumu pale anapocheza chini ya kiwango kwani siku hazifanani

Salamba amekosolewa na mashabiki wa timu hiyo kwa kushindwa kuisaidia Simba kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi iliyomalizika Januari 13 kwa Azam kutwaa taji hilo kwa kuifunga Simba mabao 2-1 kwenye mchezo wa fainali

Salamba amesema sio kweli kuwa ameshuka kiwango bali michuano hiyo haikuwa mizuri tu kwa upande wake

"Kuna wakati mchezaji unaweza kuonyesha kiwango kizuri na ukawafurahisha mashabiki lakini kuna wakati mwingine mambo huwa tofauti. Hilo ni jambo la kawaida kwa sisi wachezaji"

"Yawezekana sikucheza vizuri katika baadhi ya michezo kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi lakini hiyo haina maana kuwa kiwango changu kimeshuka. Hali hiyo imetokea tu, nafahamu jukumu langu ni kuhakikisha naisaidia timu kila ninapopata nafasi," amesema

Wakati huo huo Salamba aliyetua Simba kutoka klabu ya Lipuli Fc, huenda akaelekea nchini Ubelgiji kufanya majaribio kwenye moja ya timu zinazoshiriki ligi kuu

Salamba amesema anasubiri kukamilika kwa baadhi ya masuala baina ya timu hiyo na uongozi wa Simba ili apate ruhusa ya kwenda kujaribu bahati yake nchini humo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
12h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
12h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
15h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’