Simba haitapaki basi Congo - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Jan 2019
Simba haitapaki basi Congo - Aussems

Wakati kikosi cha Simba kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa ajili ya mchezo wao wa pili hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita, Kocha Patrick Aussems, amesema kamwe hawatacheza soka la kujilinda kwenye mchezo huo.

Aussems amenukuliwa na gazeti la Nipashe akisema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao kwa kuwa ni moja ya timu nzuri na kubwa Afrika.

“Tuna kikosi kizuri na sisi, ukitazama namna tulivyocheza mchezo uliopita utaona tunaweza kucheza soka letu na kulazimisha matokeo mazuri, hatutacheza soka la kujilinda muda wote,” alisema Aussems.

Alisema kuwa leo watafanya mazoezi ya mwishoasubuhi kabla ya kesho kuanza safari ya kuwafuata AS Vita.

Wakati Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya JS Saoura Jumamosi iliyopita kwenye uwanja wa Taifa, AS Vita wenyewe walikumbana na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Al Ahly ya Misr.

Wakati huo huo, kiungo wa Simba, Said Ndemla, leo anaanza majaribio yake kwenye klabu ya Eskilstuna baada ya kuwasili salama juzi.

Ndemla kama atafuzu majaribio atasajiliwa na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya Sweden.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’