Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kimeendelea kujifua katika uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vital Club ya Congo
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amekinoa chake kabla ya safari ya Congo ambayo inatarajiwa kuwa Alhamisi Alfajiri
Simba inatarajiwa kufanya mazoezi yake ya mwisho kesho Jumatano kabla ya safari hiyo
Mbelgiji huyo amesema anawapa wachezaji wake mbinu za kuweza kupata matokeo katika mchezo huo wa kwanza wa ugenini katika hatua ya makundi
Amesema anatambua mchezo dhidi ya AS Vital hautakuwa mwepesi kama ilivyo michezo yote ya ugenini lakini amesema watapambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri
Simba inaongza kundi D kufuatia ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya JS Saoura wakati Al Ahly iliyoichapa Vita Club 2-0 inashika nafasi ya pili
Kipigo hicho cha Vita kinaufanya mchezo dhidi ya Simba uwe mgumu kutokana na ukweli kwamba timu hiyo haitakuwa tayari kupoteza michezo miwili mfululizo.
Hata hivyo Simba inaweza ikanufaika na hali hiyo ya wenyeji kuwa katika presha ya kupata matokeo.
Ubora wa kikosi cha Simba na kujiamini kwa wachezaji wake ni sababu nyingine inayoifanya Simba isiwe na hofu kuelekea mchezo huo