Michuano ya SportPesa Super Cup inatarajiwa kufanyika nchini ikianza wiki ijayo Januari 22 na kumalizika Januari 27.
Simba, mabingwa wa Tanzania Bara wamethibitisha kushiriki michuano hiyo wakitumia kikosi cha kwanza ili kuongeza ushindani
Mapema leo SportPesa ilitangaza kuwa michuano hiyo itarushwa mbashara na televisheni ya DSTV kupitia SS9
Simba itashuka dimbani Januari 23 kuikabili AFC Leopards kutoka nchini Kenya.
Timu zote zitakazoshiriki michuano hiyo zimetakiwa kuhakikisha zinatumia vikosi vyao kamili huku timu kutoka Tanzania zikichagizwa kutumia fursa ya michuano hiyo kufanyika nchini kuweza kufanya vizuri.
Bingwa wa michuano hiyo atajinyakulia kitita cha dola 30,000 na kupata nafasi ya kucheza na Everton Fc katika mchezo utakaopigwa mwezi Julai 2019 jijini Dar es salaam