Nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco alipata majeraha kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Saoura kundi D
Katika mchezo huo ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 Bocco aliumia kwenye dakika ya 35 na nafasi yake kuchukuliwa na Meddie Kagere aliyefunga mabao mawili
Inaelezwa hali ya Bocco inaendelea vizuri hata hivyo hatma yake iko mikononi mwa Kocha Patrick Aussems iwapo amtumie kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya As Vita au la
Kikosi cha Simba kinaondoka keshokutwa Alhamisi Alfajiri kuelekea nchini Congo kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa Jumamosi, Januari 19 katika dimba la Martyrs linalochukua takribani mashabiki 80,000
Orodha kamili ya wachezaji watakaosafiri itafahamika kesho jioni baada ya kocha Aussems kumaliza program ya mazoezi ya kikosi chake