Okwi aitumia salamu Vita Club

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Jan 2019
Okwi aitumia salamu Vita Club

Jumamosi Januari 19, 2019 Simba itakuwa dimbani huko DR Congo kupepetana na AS Vita Club kwenye mchezo wa raundi ya pili ligi ya mabingwa, kundi D

Mabingwa hao wa Tanzania wanatarajiwa kuondoka keshokutwa kuelekea Congo tayari kwa mchezo huo.

Mshambuliaji wa Kimataifa Mganda Emmanuel Okwi amesema ataendeleza makali yake katika michezo yote atakayoshuka dimbani na kikosi cha Simba

Katika mchezo dhidi ya JS Saoura Okwi alihusika katika mabao yote ya Simba alifunga bao moja na kutengeneza mengine mawili yaliyofungwa na Meddie Kagere

Okwi amebainisha kuwa baada ya kupona majeraha yaliyokuwa yakimuweka nje mara kwa mara, ataendelea kuipigania Simba kila atakapopewa nafasi na kocha Patrick Aussems

"Kwa sasa nipo fiti na nitaendelea kupambana kwa ajili ya timu yangu, nilikuwa nashindwa kufanya vizuri kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mgongo ila kwa sasa maumivu yamekwisha ni mwendo wa kazi tu," amesema Okwi.

Simba inaongoza kundi D ikiwa na alama tatu na mabao matatu ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama tatu na mabao mawili

AS Vital Club na JS Saoura zilifungwa katika michezo ya raundi ya kwanza hivyo hazina pointi

Wakati Vita Club ikiikaribisha Simba Jumamosi, Ijumaa JS Saoura itapepetana na Al Ahly nchini Algeria

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’